Thursday 9 November 2017

JE UNAJUA FAIDA YA MACHUNGWA MWILINI

Habari yako ndugu msomaji .Swala la Afya bora  ni jambo muhimu sana katika Maisha ya kila mmoja wetu na taifa kwa ujumla. Bila afya hakuna furaha,amani wa shughuli yoyote ile ya maendeleo.Afya ndio msingi wa maisha yetu ya kila siku.
Upuuziaji wa matumizi ya matunda na mboga mboga unachangia kwa kiasi kikubwa matatizo mengi ya kiafya. Matunda ni moja ya zawadi kutoka kwa Mwenyezi Mungu binadamu tuliopewa japo tunaidharau licha ya faida yake katika maisha yetu. leo nimekuletea tunda hili nikujuze faida zake
Haya ni matunda matamu sana ,rahisi sana kupatikana na yenye faida nyingi mno kwa afya yako.Matunda hayab hupatikana kwa wingi bila gharama kubwa  mfano kwa wale waliofika Morogoro na Tanga  wanajua uwingi wa matunda haya. kama hujui tazama virutubisho muhimu sana viliyomo katika machungwa.
  • Vitamin C   __________________ 93%
  • Fiber             __________________ 13%
  • vitamini B1 __________________  9%
  • Pottasium   __________________  7%
  • Calcium      ___________________  5%
Na virutubisho vingine vingi sana huku  vikiwa na faida muhimu zaidi ikiwemo:
  • Vitamic C ya machungwa husaidia kuimarisha  ulinzi wa Antioxidant na ulinzi dhidi ya magonjwa
  • Machungwa husaidia kuzuia ugonjwa wa mawe katika figo(kidney stones)
  • Machungwa huzuia kansa na vidonda vya tumbo
  • Machungwa husaidia na kuboresha  afya ya mfumo wa upumuaji.
Yapo mengi na faida nyingi sana za machungwa Pia inashauliwa wakata unatumia tunda hili 60% ya  vitamin vilivyopo katika tunda vipo kwenye kuta za ndani nyeupe raini zipo kama nailoni na 40% ipo katika majimaji yake  hili kupata 100% ya vitamini ya kila chungwa ni vyema zaidi kula Chungwa na kulinyonya ni bora kuliko kutumia juisi yake tu
  Natumaini utakua umenielewa ndugu msomaji nakutakia siku njema pia usikose kutembelea blog hii kila siku hili kujua mengi zaidi kula machungwa
mara kwa mara uone faida yake kwa afya yako.

0 comments:

Post a Comment