Thursday, 9 November 2017

JE UNAJUA HISTORIA YA MWANADADA SHILOLE

Amezaliwa Igunga Tabora Mwaka 1987 tarehe 6 mwenzi 12. Jina lake la passport ni Zuena Mohamed . Baba yake alimkimbia mama yake akiwa akitambaa na alikuja kuambiwa na ndugu zake baba yake alipata matatizo ya akili ila hajawahi kuonana naye.
Alisoma shule ya msingi Igunga na alifaulu kwenda Igunga sekondari ila aliishia kidato cha pili baada ya kubakwa na kubeba mimba akiwa na miaka 14. Huyo mtu aliyefanya kitendo hicho alikutana naye akiwa anaenda kuchota maji kisimani na kufanya hicho  Mtoto alizaliwa anaitwa Joyce kwa sasa anamiaka 11.

Baada ya hapo alianza kutafuta riziki akawa akifanya biashara za kuuza mikate na maji stendi ya Igunga kipindi hicho alikuwa na miaka kumi na tano, pia alikuwa akitembeza mikate katika nyumba za watu. Baadaye alifungua genge lake na kupanga chumba chake ambacho alilipa 3000 kwa mwenzi alifanya hivyo kwa miaka miwili.
Alipata bwana ambaye alikuwa anaendesha magari makubwa aliposwa na kuolewa naye akiwa na miaka 16. Alimchukua na kwenda kuishi naye Dar es Salam kwenda kishi naye ilikuwa mwaka 2005 walishukia gesti mitaa ya Keko kwa muda ndipo mwanaume alitafuta nyumba ya kupanga na kuanza kuishi na Shilole.
Alimpa ujauzito na kujifungua salama tangu hapo ndipo mume wake alianza kubadili tabia. Mwanaume aliyemuoa alimzidi Shishi kwa miaka kumi. Mume wake alianza kumpiga sana hadi ilifika hatua Shilole anaenda kulala na watoto wake katika kituo cha polisi  Keko.Shilole alianza kusoma hotel managment japo mume wake hakutaka na alihitimu masomo yake na kufaulu kisha alipangwa kazi sehemu ya Pikoku hotel. Baada ya mume wake kuona hivyo alimwandikia talaka na kumtolea vitu vyake nje.BabaSiku moja Ray alikuja Hotelini hapo Shishi alimuhudumia Ray alipenda uchangamfu wake Shishi na Shishi alimwambia Ray kwamba anapenda kuigiza. Alikwenda kwenye mazoezi Ray alimpa mtihani wa kumtongoza Shishi aliweza na kumruhusu ashiriki katika filamu ya Fair decision na mlango wa shilole ulifunguka katika filamu.
Shilole alikutana na Q Chief na kumwambia kwamba anaweza kuimba walienda koko beach kwa ajili  na kumpima Q chief alimkubali na kuamua kumchukua na kumpeleka kwa C9 na kufanya nyimbo ya ‘lawama’ nyimbo ikawa pouwaa akaenda clouds akakutana na Ruge akampa moyo na support ya kutosha katika shoo mbalimbali bongo Pia alishawahi kuonekana kama video queen kwenye nyimbo kadhaa kama SABABU YA UROFA.nk shilole sasa ni msanii mkubwa Tanzania na nchi kadhaa za africa zinamjua kwa nyimbo zake Nakomaa na jiji ,na hatutoi kiki  kwa bahati mbaya  hakubahatika kupata tuzo Alishawahi kua na mahusiano na Msanii wa muziki mwenzake Nuh Mziwanda

0 comments:

Post a Comment